Sallam SK afunguka Diamond kupotezwa.

Meneja wa msanii wa muziki Diamond Platnumz, Sallam SK amefunguka kwa kudai kwamba kuna watu wanataka kumshusha msanii huyo ambaye anafanya vizuri kwa sasa na wimbo, ‘Waka’ aliomshirikisha Rick Ross.

Sallam amedai kwamba hakuna mtu wakumshusha muimbaji huyo kwa hasa hasa kwenye utawala huu wa Rais John Pombe Magufuli.

“Kumbe tatizo ni kumpoteza huyu kijana?(Diamond) Waambie familia yako na wazazi waliyokuleta katika haya maisha huyu mtoto kaletwa kwa makusudi maisha haya, ili kuleta ukombozi wa dhuluma uliyokuwa unaleta kwenye Taifa hili, unatakiwa kujua Kwanza hili Taifa sasa Rais anaitwa John Pombe Magufuli,” aliandika Sallam kupitia instagram yake.

Habari ambazo zipo mtaani zinadai kwamba wasanii wa label hiyo hawapati airtime kama kipindi cha nyuma hali ambayo inatishia biashara ya wasanii hao.