Waislamu wa Chanika Zingiziwa wapata neema (Picha)

Miongoni mwa nguzo ya dini ya kiislamu moja wapo ni kutoa zakka (sadaka),ambapo kitendo hicho mja (Binaadamu) hupandishwaa Hadhi na Mola wake hali ambayo kwa dini ya kiislamu huamini kutoa sadaka ni kitendo ambacho pia hufuta madhambi na kusamehewa kabisa.

Sheikh Sultan Said (Kulia ) akiwa ameshikilia picha ya mfano wa Msikiti utakavyokuwa mara baada ya Kukamilika.

Kitendo hicho kimejidhihirisha mapema leo jijini Dar es salaam ,ambapo mfadhili mmoja kutoka nchini Oman Sheikh Sultan Ryami, amejitolea kujenga Msikiti utakaoweza kuchukua zaidi ya Waislamu mia tano katika Eneo la Chanika Zingiziwa.

Akizungumza Jumapili hii Sheikh Nassor Jahadhmi kutoka nchini Oman amesema wamekuja mara hii kuweka Jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Msikiti huo Mara Moja katika eneo la hilo Jijini Humo, ambapo Msikiti huo utajumuisha Maduka,Nyumba ya IMam ,Pamoja na nyumba ya Mayatima,na sehemu ya Kuoshea Maiti.

“Katika eneo hilo pia tutajitahidi kuweka Madrasa kwa ajili ya watoto kujifunza imani yao ya dini ya kiislam na pia msikiti huo utakuwa na sehemu ya kuswalia wanawake pia tunaomba mwenyezi mungu Subkhanahu wataala aikubali Swadaka hii kwa waliotoa Mwenyezimungu awabariki,” amesema Sheikh Nassor.

Msikiti huo unategemea kughalimu kiasi cha Shilingi Milioni Mia Moja na ishirini na Tano na ujenzi huo utaanza ndani ya miezi mitatu ijayona kutegemea kukamilika mpaka ifikapo Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Mradi huo Sheikh Naadir Mohammed Mahfudh amesema madhumuni ya ujenzi huo pia utachangia kuinua imani za watu na kuwasaidia watoto kuweza kuwakuza katika Maadili mema ayapendayo Mwenyezimungu.

Naye mfadhili wa Mradi huo Sheikh Sultan Bin Muhamed Bin SAID Riyami ,amesema ujenzi huo utamfurahisha Mwenyezimungu vile vile itakuwa ni alama kwa watu wengine kufuata nyao zake na hatimae kuchangia ili kuendeleza Dini ya hiyo.

“Watu wenye uwezo Mnapoona kitu kama hiki ni heri mkakichangamkia kwani itakuwa ni kheri kwenu na mbele ya MwenyeziMungu na kuweza kuwabariki katika maisha yenu ya akhera na Duniani”.Amesema Sheikh Surtan


Sheikh Nadir akizungumza na Waandishi wa HABARI Mara baada ya kutembelea eneo hilo.


Mfadhili huyo, Sheikh Nassor Jahadhmi akionyeshwa eneo lililonunuliwa kwaajili ya ujenzi wa Msikiti huko Chanika Zingiziwa Jijini Dar es salaam leo.