Okwi, Bocco waibeba ‘Simba SC’ Taifa

Klabu ya Simba leo Jumapili Januari 28, 2018 imefanikiwa kupata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Majimaji FC ya Songea katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Kutoka kulia John Bocco na Okwi wakishangilia .

Magoli ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi goli mbili na John Bocco naye akitupia goli mbili.

Kwa matokeo hayo ya mzunguuko wa 15 wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara, Simba inabaki kileleni kwa alama 35 ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 30.

Matokeo mengine ya mechi za leo ni Singida United imeshinda goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya jijini Mbeya.