Daktari ahukumiwa miaka 175 jela.

Aliyekuwa daktari wa timu ya Olimpiki Larry Nasser amehukumiwa kwenda jela miaka 175 baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi wananawake na wana michezo.

Katika kesi hiyo mashahidi 160 wamewasilisha ushahidi wao huku Nasser mwenyewe alikiri makosa kumi.

Alikuwa tayari akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha ngono za watoto kinyume cha sheria.

Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama kuwa amejisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa wengine.

‘Nataka ukae jela maisha yako yote’. Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mmoja wa waathirika amesisitiza kuwa washirika wa daktari huyo wanapaswa kushitakiwa pia.

Muda mfupi baada ya kutolewa hukumu hiyo, mkuu wa chuo kikuu cha jimbo la Michigan (MSU) alikokuwa anafanya kazi Nassar kati ya mwaka 1997 na 2016, amejiuzulu.