MCB ya Selementally yasambaratika, Rogers atimka.

Studio ya MCB (Mbeya City Banger’s) chini ya usimamizi wa msanii Selementally zimepata pigo baada ya Producer wao Rogers Model kubwaga manyanga.

Akiongea na TogoroMedia.com, Rogers ameweka wazi sababu za yeye kuondoka MCB ikiwa ni pamoja na kutopewa thamani yake kama Producer ambaye ameipa jina studio hiyo kwa kuandaa ngoma kali kama vile “Nataka kuinunua  Dar” ya Selementally Ft Belle 9 na “Tunagongea” ambayo pia inafanya vizuri kwa sasa.

Pia Rogers ametoa sababu nyingine kuwa akiwa kama Producer hajawahi kuzungumziwa na Selementally kwenye interviews zake kinyume na yeye anavyofanya akiwa katika media mbalimbali kuzungumza kuhusu kazi yake.

Rogers amesema ameamua kurudi kwako Dar kuangalia maisha mengine na kwamba yuko huru kufanya kazi na studio yoyote itakayomuhitaji.