Blac Chyna awatamanisha wanaume kwa gauni lake.

Blac Chyna ni mmoja kati ya wasichana wanaotupia pamba za kufa mtu na zikampendeza. Mrembo huyo ambaye amebarikiwa kuwa na umbo la kumchanganya kila mwanaume aliyekamilika amewashtua mashabiki mitandaoni kutokana na gauni lake alilovaa katika kipindi cha kusherehekea sikukuu ya Christmas pamoja na kuuaga mwaka 2017.

Chyna amepigilia gauni hilo lenye rangi nyekundu na mpasuo mpaka karibia na kiuno, limeonekana kumkaa kisawa sawa mrembo huyo mwenye miaka 29 na kuonekana kigori huku akisahaulika kabisa kama ni mama wa watoto wawili. Je kwa mtazamo wako unampa asilimia ngapi kwa gauni hili?