Bushoke na Papii Kocha kusikika kwenye wimbo mmoja.

Baada ya muimbaji, Papii Kocha kurudi uraiani na kukutana na rafiki yake Bushoke, wawili hao wanajipanga kuingia studio kwa ajili ya kuandaa kazi mpya za muziki.

Bushoke amesema amefurahi sana rafiki yake huyo kuwa huru huku akiahidi kuanza kufanya mchakato wa kumrudisha kwenye game rasmi.

“Nafikiria kufanya naye kolabo,” Bushoke aliliambia Gazeti la Mwanaspoti. “Mungu akijalia ziwe nyingi,  nikifanya shoo napenda ashiriki na vitu vingi napenda nimsaidie ila siwezi kuviweka wazi,”

Ikumbukwe kuwa Bushoke ndiye msanii wa Kwanza kabisa kufanya harakati za kumtetea Papii Kocha kupitia wimbo wake wa “Msela” ambao aliuimba mara baada ya Papii kuhukumiwa kifungo cha maisha Jela.

Papii Kocha pamoja na baba yake waliachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Pombe Magufuli.