Kibabage, Makame rasmi Njombe Mji.

Klabu ya Mtibwa Sugar imewaruhusu nyota wake wawili Nickson Clement kibabage na Muhsin Makame Malima kujiunga na kikosi cha Njombe Mji kwa mkopo wa miezi sita.

Mchezaji wa klabu ya Mtibwa Sugar na timu ya Taifa ya Serengeti Boys, Muhsin Makame Malima 

Nickson Clement Kibabage anayemudu kucheza mlinzi wa pembeni na Muhsin Makame Malima anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wamejiunga na kikosi cha timu ya Njombe Mji kutoka katika mkoa wa Njombe.

Kwa takribani wiki moja wachezaji hawa wa kikosi cha Mtibwa Sugar walikuwa katika majadiliano na uongozi wa Njombe Mji na hatimaye makubaliano yamefikiwa na pande zote tatu ambazo ni wachezaji wenyewe , Klabu ya Mtibwa Sugar na Njombe Mji.

Wachezaji hawa waliokuzwa katika Academy ya Mtibwa Sugar yenye mskani yake Manungu wamejiunga na Njombe Mji kwa mkopo wa miezi 6 hivyo wachezaji hawa watadumu katika kikosi hicho hadi mwisho wa msimu huu wa 2017/2018.

Muhsin Makame Malima na Nickson Clement Kibabage ni kati ya vijana waliowakilisha taifa katika michuano ya AFCON chini ya miaka 17 kwa mara ya kwanza.