Klabu Bingwa Afrika, Yanga kuanza nyumbani.

Droo ya michezo ya awali ya michuano ya ngazi za klabu imetangazwa rasmi na Shirikisho la Soka Afriaka (CAF) ambapo imefanyika katika makao makuu yake huko Jijini Cairo Misri.

Jumla ya mashirikisho 59 yameshiriki katika michuano ya Klabu Bingwa  mwaka 2018 huku 54 yakishiriki kwa upande wa kombe la shirikisho.

Wakati mashirikisho nane pekee yakishindwa kushiriki ambapo timu zao ni pamoja na Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome na Principe, Sierra Leone pamoja na Somalia.

Klabu ya soka ya Yanga itaanza nyumbani katika mchezo wake wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika kwa kuikabili timu ya St. Louis.

Kuangalia ratiba Klabu Bingwa Afrika  Bofya HAPA

Kwa upande wa klabu ya Simba ambayo itaiwakilisha nchi kupitia kombe la Shirikisho Afrika imepangwa kucheza na Gendarmerie Tnale huku nayo ikianzia nyumbani katika mchezo wake wa kwanza.

Kuangalia ratiba Kombe la Shirikisho Bofya HAPA