The Rock atarajia kupata mtoto mwingine.

The Rock ametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuweka picha ya Binti yake Jasmine Lia na kusema kuwa ana jambo la kusema huku nyuma yake kukiwa na bango dogo lenye maandishi kiliashiria kuwa kuna mtoto anatarajiwa kuzaliwa wa kike.

Dwayne na Laurene wamekuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda wa miaka 10, Na amekuwa baba bora kwa binti yake Simone Johnson (16) .